Wednesday, 11 May 2016

Infectious Bronchitis Virus (IBV)

UTANGULIZI

Infectious Bronchitis Virus (IBV) Ni ugonjwa uambatanao na mafua makali pia hushambulia zaid mfumo mzima wa upumuaji katika rika na makundi yote ya kuku. 
 madhara makubwa hujitokeza katika mfumo mzima wa upumuaji, kama mapafu,bandama na husababisha vifo vingi na kuku hukata kutaga mayai kwa 95% kutokana na madhara katika mfumo mzima wa ovari(tezi za mayai).
MAAMBUKIZI
Virusi hivi huenea baina ya kuku wa kundi moja na lingine na maambukizi hutokana na kinyesi chenye vimelea ,chafya na kikohozi cha kuku,
ZINGATIO
Ueneaji wa ugojwa huenea kati ya banda moja na lingine kwa njia ya upepo endapo mabanda yanakaribiana na banda lenye maambukizi.
Kuku mwenye maambukizi anakuwa amebeba ugonjwa na ni hatarishi kuambukiza kundi lingine jipya la kuku.
Maambukizi kwa kifaranga katika wakati wa uanguaji huanza kuonesha dalili za awali na ugonjwa kudhihirika baada ya saa 18 hadi 36 kwa majibu ya vipimo upasuaji(post surge results) .  
kuku mwenye maambukizi hudhoofu na utagaji hupungua kwa kasi na wakati mwingine kuku aliebeba maambukizi huwa mwenezi kwa kuku wengine. ugonjwa huu maambukizi yake huenea baina ya kuku na hauadhiri mayai. hivyo maambukizi haya hayahusiani na yai wala menejimenti ya uzalishaji.























martfowls consults
0688 977 000, 0679 666 534.
martfowls89@gmail.com

No comments:

Post a Comment