martfowlspoultry
Tuesday, 26 June 2018
Dodoma Kuku project
We expand the project to Dodoma as the poultry consults and raring advisers, (Sasa tupo Dodoma kumfikia Mfugaji na kushauri njia asili na kisasa Katika malezi na jinsi ya ufugaji Kuku.
Wednesday, 11 May 2016
Infectious Bronchitis Virus (IBV)
UTANGULIZI
Infectious Bronchitis Virus (IBV) Ni ugonjwa uambatanao na mafua makali pia hushambulia zaid mfumo mzima wa upumuaji katika rika na makundi yote ya kuku.
madhara makubwa hujitokeza katika mfumo mzima wa upumuaji, kama mapafu,bandama na husababisha vifo vingi na kuku hukata kutaga mayai kwa 95% kutokana na madhara katika mfumo mzima wa ovari(tezi za mayai).
MAAMBUKIZI
Virusi hivi huenea baina ya kuku wa kundi moja na lingine na maambukizi hutokana na kinyesi chenye vimelea ,chafya na kikohozi cha kuku,
ZINGATIO
Ueneaji wa ugojwa huenea kati ya banda moja na lingine kwa njia ya upepo endapo mabanda yanakaribiana na banda lenye maambukizi.
Kuku mwenye maambukizi anakuwa amebeba ugonjwa na ni hatarishi kuambukiza kundi lingine jipya la kuku.
Maambukizi kwa kifaranga katika wakati wa uanguaji huanza kuonesha dalili za awali na ugonjwa kudhihirika baada ya saa 18 hadi 36 kwa majibu ya vipimo upasuaji(post surge results) .
kuku mwenye maambukizi hudhoofu na utagaji hupungua kwa kasi na wakati mwingine kuku aliebeba maambukizi huwa mwenezi kwa kuku wengine. ugonjwa huu maambukizi yake huenea baina ya kuku na hauadhiri mayai. hivyo maambukizi haya hayahusiani na yai wala menejimenti ya uzalishaji.

martfowls consults
0688 977 000, 0679 666 534.
martfowls89@gmail.com
Tuesday, 10 May 2016
controler installation
Martfowls tunarekebisha device na kufunga mifumo ya kisasa kwa incubator zenye muonekano wa kizamani eg. turner motor, auto controler, humidifier na vifaa vinginevyo vinavyokamilisha mfumo mzima wa machine
Thursday, 5 May 2016
Kuku: Jogoo na tembe
Ulishaji:
Kuku wa kienyeji wanaweza kulishwa kwa kumia mahindi, mchele, na mabaki ya ugali. Vyakula hivi ni lazima vikaushwe vizuri na kusagwa vizuri. Ulishaji ni lazima ufanyike katika sehemu safi au kwa kutumia vyombo vilivyotengenezwa maalumu kwa ajilii ya kulishia kuku.
Banda:
Kuku wawe wa kienyeji au wa kisasa, wanahitaji kuwa na banda zuri kwa ajili ya malazi na kuwalinda. Wanahitaji chumba chenye nafasi ya kutosha na kinachopitisha hewa ya kutosha. Ni lazima kuwawekea fito kwa kuwa ndege hupenda kupumzika juu ya fito. Ni lazima banda la kuku lifungwe vizuri nyakati za usiku ili kuzuia wanyama wanaoweza kuwadhuru kuku. Ni lazima liwe safi wakati wote ili kuzuia magonjwa kama vile mdondo na mengineyo. Usitumie pumba za mbao au nguo kuukuu kwenye viota vya kutagia kwani huchochea kuwepo utitiri na funza wa kuku. Inashauriwa kutumia mchanga laini.
Maji ya kunywa:
Kuku wapatiwe maji safi. Ni lazima kuangalia mara kwa mara na kuyabadilisha maji. Kamwe usiwape kuku maji machafu.
Chanjo:
Chanjo kwa mifugo ni lazima ili kuzuia mashambulizi ya magonjwa. Magonjwa yaliyozoeleka ni kama vile Mdondo, Kideri, Ndui ya kuku, na homa ya matumbo (typhoid). Chanjo kwa kawaida hutolewa mara moja kwa kila baada ya miezi miwili.
Uwekaji wa kumbukumbu: Kumbukumbu zijumuishe aina ya ulishaji, namba ya uzalishaji, muda wa mwisho wa matumizi, kiasi cha malisho kwa kila siku, idadi ya vifo, na idadi ya mayai yaliyozalishwa.
Mwanzoni unahitaji nini?
Wafugaji walio wengi wanauliza wanahitaji nini katika hatua za awali ili kuweza kuanzisha mradi wa ufugaji wa kuku. Hii itategemea aina ya kuku uliochagua kufuga.
Ni busara kuwa na vifaa muhimu vinavyohitajika na viwe katika hali ya usafi kabla ya kuweka kuku bandani mwako. Kama unaanza na vifaranga, vifuatavyo ni vifaa muhimu vinavyohitajika kwa ajili ya vifaranga 200.
• Tenga na utengeneze banda zuri lenye joto na hewa ya kutosha wakati wote.
• Vyombo vinne (4) vya kunyweshea maji, hii ni katika wiki 2 za mwanzo na uongeze vyombo taratibu kulingana na kuku wanavyokua.
• Vyombo vinne (4) vya kulishia chakula, na viongezeke kulingana na kuku wanavyokua.
• Matandazo makavu na safi, inaweza kuwa maranda au mabua ya ngano.
• Pakiti moja au mbili za dawa ya Coccid (hii inapatikana katika maduka yote ya kilimo). Hata hivyo, utaratibu wa chanjo ni lazima ukamilishwe.
• Chakula kwa ajili ya vifaranga ambacho kimezalishwa na watengenezaji wanaoaminika.

chanzo.
martfowls poultry consults
0688 977 000
0679 666 534
poultry consultants and maintanance
Tunafanya matengenezo ya incubator na kutoa ushauri wa kitaalamu kwa wazalishaji,
furmigators and distributors of incubator parts
furmigators and distributors of incubator parts

INCUBATORS
Tunatoa ushauri wa kitaalamu kwa wazalishaji vifaranga,
tunatengeneza machine(incubator) kwa gharama nafuu,

tunatengeneza machine(incubator) kwa gharama nafuu,

poultry consultants
Tunatoa Ushauri kwa wafugaji na maelekezo dhubuti ya ufugaji kuku wenye tija katika kuongeza kipato cha mfugaji, pia tunazalisha na kusambaza vifaranga, toka katika farm project yetu iliyopo Arusha.
Subscribe to:
Posts (Atom)